Ushindi usipopatikana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Mithali 3:5,7 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.
Kuna nyakati mtu anaweza kukumbana na matukio magumu na mazingira hatarishi kiasi kwamba hajui afanye nini. Na tukisema kweli, mara nyingi tunadhani kwamba uwezo wa kutatua matatizo na kutoka upande wa pili wa hali hiyo ni ushindi. Lakini katika maisha, si kila wakati tutashinda—hapana.
Dada Jane Haining alikuwa mishonari kutoka Scotland aliyekuwa akihudumu nchini Hungary. Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia, alikataa kuwaacha wasichana wa Kiyahudi aliokuwa anawalea. Alipoagizwa na misheni kurudi nyumbani kwao, aliandika kwa kujibu: “Kama watoto hawa walinihitaji wakati wa hali nzuri ya hewa, si zaidi siku hizi zenye giza?”
Mwaka 1944, alikamatwa na upelelezi wa Ujerumani na kupelekwa katika kambi ya maangamizi ya Auschwitz, ambako alifariki. Alipokumbana na changamoto nzito na kukosa kujua afanyeje, alimtegemea Kristo pekee. Miaka mingi baadaye, aliheshimiwa na taifa la Israel kwa kutajwa miongoni mwa Waadilifu Kati ya Mataifa. Huenda hakujua majibu yote, lakini Mungu hakushindwa kamwe. Utulivu wa imani yake uliendelea hata wakati hakuelewa kabisa kilichokuwa kinaendelea.
Sasa mtu anafikaje kwenye msimamo huo? Wewe na mimi, tunataka kushinda—kwa kweli! Tunataka kushinda utambuzi wa ugonjwa wa kansa. Hatutaki benki kuiweka hati miliki ya kiwanja chetu kwenye mnada wakati tunapitia hali ngumu ya kiuchumi na kushindwa kulipa deni kwa wakati. Lakini vipi kama ushindi hautapatikana? Itakuwaje basi?
Mithali 3:5,6
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.
Ni lazima mtu ajitahidi kushinda matatizo yake pale inapowezekana. Lakini mambo yanapokuwa juu ya uwezo wako, tuliza mawazo yako na usitegemee akili zako mwenyewe. Kama ni mapenzi ya Mungu, basi yatatimia. Na kama si mapenzi yake, basi Mungu ana mpango ulio bora zaidi. Uwe na amani kwa kujua hilo, kwa sababu—atayanyosha mapito yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.
