Helping you live the life God intended

Tumaini Lililo Hai

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 1:3 Ahimidiwe Mungu, baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.

Listen to the radio broadcast of

Tumaini Lililo Hai


Download audio file

Maisha huweza kuchosha. Iwe ni kwa sababu ya marudio yasiyoisha, au mivutano iliyo nje ya uwezo wako, kuna siku sisi sote hukosa tumaini kabisa. Je, mtu afanye nini?

Mimi binafsi nina “kazi” yenye baraka kuliko zote duniani—kama kweli naweza kuiita kazi. Ni kushirikisha Habari Njema ya Yesu kwako na kwa wengine wasiohesabika, siku 365 kwa mwaka. Hii ni kazi niliyoumbwa kuitimiza.

Lakini yapo masiku ambayo hata mimi sijisikii vizuri. Huenda ninaumwa kidogo, au ugonjwa wa kansa anaopambana nao mjukuu wangu wa kike unanilemea moyoni, au kalenda ya kuandika na kuandaa vipindi mbalimbali inanitia hofu. Usinielewe vibaya—ninapenda sana kazi ninayofanya. Lakini maisha, bila shaka, hayakosi changamoto mara kwa mara—kwangu mimi na kwako pia.

Siku hizi tumekuwa tukisimulia habari ya ajabu na ya furaha kuu ya ufufuo wa Yesu Kristo. Na kwa kuwa Pasaka ilikuwa juzi tu, hilo linaeleweka. Lakini swali linabaki: je, mtu anawezaje kuunganisha habari hiyo na uhalisia wa maisha yake, pamoja na changamoto anazokabiliana nazo leo?

1 Petro 1:3
Ahimidiwe Mungu, baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.

Wakati mtu anaweka imani yake ndani ya Kristo, ufufuo wake humpa zawadi kubwa sana—yaani, kuondolewa hukumu na kupewa maisha mapya, kuanzia sasa hadi milele. Rafiki yangu, hapo ndipo palipo kiungo muhimu, kwa sababu maisha haya mapya yanakuingiza katika tumaini lenye uzima, kupitia ufufuo wa Yesu Kristo kutoka kwa wafu.

Katikati ya changamoto zako zote, tumaini hili hurudi tena na tena. Linakuwa hai ndani yako kila dakika ya kila siku. Haliwezi kufa, kwa sababu katika Kristo, ni tumaini lenye uzima.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy