Helping you live the life God intended

Kwaheri Kiburi, Karibu Yesu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wagalatia 2:20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu

Listen to the radio broadcast of

Kwaheri Kiburi, Karibu Yesu


Download audio file

Tuwe wazi. Ni mara ngapi ubinafsi wako umekupelekea kujidanganya na kufuata njia ya hatari inayoishia kwenye uharibifu? Labda utafikiri ninapiga chuku, lakini ukweli ni kwamba kiburi cha ubinafsi ndicho mara nyingi huongoza watu.

Mwaka 2003, akiwa na umri wa miaka 19 tu, Elizabeth Holmes alianzisha kampuni ya teknolojia ya afya iitwayo Theranos mjini Palo Alto, mkoani California, Marekani—katikati ya makampuni makubwa ya teknolojia. Kampuni hiyo iliahidi kuleta mapinduzi makubwa katika vipimo vya damu. Kupitia juhudi kubwa na ushawishi mwingi, Holmes alijitengenezea taswira ya kufanana na Steve Jobs, mwanzilishi wa kampuni ya Apple.

Hata hivyo, nyuma ya mwonekano huo wa kuvutia kulijificha udanganyifu mkubwa. Wakati watu walianza kubaini kwamba mambo hayakuwa sawa, badala ya kukiri mapema kuwa amefeli kwa kiasi fulani, kiburi chake kilimsukuma kuendelea kudanganya wawekezaji, wagonjwa, na umma kwa ujumla.

Baada ya thamani ya kampuni yake kufikia dola za Kimarekani bilioni 9, Theranos iliporomoka ghafla kufuatia uchunguzi wa vyombo vya habari mwaka 2015 uliobaini utapeli huo. Kilichoanza kama maono na juhudi kubwa, kiligeuka kuwa kiburi tupu. Kama Holmes angejinyenyekeza mapema, huenda angeepuka hasara kubwa. Lakini kiburi kilimlazimisha aonekane amefaulu kwa gharama yoyote.

Sikiliza alivyoandika Mtume Paulo:

Wagalatia 2:20
Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Kwaheri kiburi, karibu Yesu. Ni kweli kabisa, kuna gharama katika kujitoa na kumkaribisha Yesu kama Bwana—kukubali utu wetu wa kale usulubiwe pamoja na Kristo. Niseme wazi: inaumiza.

Lakini kinachofuata ni uhuru—uhuru kutoka kwenye ubinafsi, kuachana na kiburi, na kuepukana na uharibifu wake. Hapo ndipo tunaweza kuishi kwa imani ndani ya Mwana wa Mungu, aliyetupenda na kujitoa kwa ajili yetu.

Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy