... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Zidi Kumtafuta Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 9:10 Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.

Listen to the radio broadcast of

Zidi Kumtafuta Mungu


Download audio file

Sawa, unaendelea na shughuli zako za kila siku, ukifanya kazi kwa nguvu na kujaribu kuishi maisha kama inavyotakiwa.  Unajaribu pia kutimiza matazamio ya watu wote wengine; na kujaribu, kama unao mwelekeo huo, kuishi sawa na matazamio yake Mungu.

Ni safi kabisa.  Ndivyo inavyotakiwa iwe.  Jana, kama uliweza kufuatana nasi, tulikuwa na masimulizi kwamba hata kama nafsini mwako umechoshwa kiasi cha kutaka kuacha kabisa, bado unahitaji kuajibika, kupiga hatua – moja, mbili, tatu; na kuendelea na kazi Mungu aliyekupa uifanye hapa duniani.  Lakini hakuna aliyesema kwamba utaendelea peke yako, hapana.

Zaburi 9:10  Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.

Sijui unapokeaje ujumbe huu, lakini mstari huu unanichangamsha kabisa.  Unasabisha ni inue macho yangu kutoka chini kwenda juu nitazame ukuu wa enzi na utukufu wa Mungu ambaye wakati ninazidiwa na uzito wa taabu zangu, anafungua mlango ili niweze kumkimbilia – yeye Muumba Mbingu na Nchi – ili nisalimike, nifarijike, nipate ulinzi.

Tuvute pumzi kwanza kwa kutulia ili tuweze kuyatafakari kidogo.  Mungu yu pamoja nawe hapa hapa.  Mlango wake ni wazi … kwa ajili yako!  Ukimjia, hawezi kuacha kukusaidia wewe umtafutae!

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.