... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Zawadi Inayoendelea Kuleta na Zingine

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 5:24 Amin, amni, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

Listen to the radio broadcast of

Zawadi Inayoendelea Kuleta na Zingine


Download audio file

Ninakumbuka zamani wakati wale Wakristo walikuwa wanaongea habari za Yesu na dhambi na msamaha na “kuokolewa”, na uzima wa milele na mengine mengi, kwangu ilikuwa kama hayanihusu hata kidogo – katika maisha yangu ya wakati ule – kwamba walikuwa kwangu kama wageni kutoka sayari ingine.

Haijalishi unaamini nini – labda unajiita Mkristo, labda wewe si Mkristo – lakini kwa vyo vyote, kadiri unazidi kupambana na maisha na changamoto zake, ndipo mambo yale yote ya Ukristo yanazidi kuonekana kwamba hayakuhusu ukikutana nayo.  Labda ndiyo hali yako ilivyo leo.

Lakini hata zamani, wakati Yesu alikuwa hapa duniani, maisha yalikuwa magumu jamani.  Wakulima wanaoishi kwa kilimo chao kwa shida.  Ukoloni wa udikteta wa Kirumi wenye ukatili pamoja na viongozi manafiki wa dini waliokuwa wanazidisha masharti na kanuni juu ya zingine na kulemea watu na makatazo mengi sana.

Ni katika mazingira kama hayo, Yesu aliweza kutamka maneno yafuatayo:

Yohana 5:24  Amin, amni, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.

Uzima wa milele unaoanza leo hii, hapa hapa.  Uzima wa milele utakaotuongoza kupitia raha na changamoto zote tunazokabiliana nazo.  Uzima wa milele wakati tutavuta pumzi kwa mara ya mwisho, na kuvuka mauti, na huzuni, na machozi na maumivu.  Uzima wa milele mbele za Mungu mwenyewe, milele na milele.

Huyu Yesu.  Msikilize.  Mwamini.  Yeye ndiye zawadi inayozalisha na zingine.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy