... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Yesu Alikuja Ili …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Yohana 3:8 Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

Listen to the radio broadcast of

Yesu Alikuja Ili …


Download audio file

Ninawiwa leo niongee na wewe kuhusu jinsi ulioweza kuridhiana na mambo madogo maishani mwako.  Yaani, dhambi zile “ndogo-ndogo” ambazo unadhani kwamba hazina tatizo, zile unazoficha wengine wasizione.

Mungu hatenganishi “dhambi kubwa” na “dhambi ndogo”.  Katika Wagalatia 5:19 anajumlisha kwa orodha yafuatayo:  uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, na ulafi. 

Kwa hiyo kusababisha ugomvi kazini ni dhambi kama vile ulevi na ulafi.  Hakuna utofauti.  Kwa hiyo, tuache kujidanganya kwamba tunaweza kunusurika kwa kuridhiana na mambo ambayo Neno la Mungu linayataja kuwa ni dhambi. 

Sikiliza mstari huu … 

1 Yohana 3:8  Atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo.  Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 

Jamani, ni mstari wenye tafakuri unaopenya na kuweka bayana maridhiano tunaojaribu kuyatolea udhuru.  Je!  Umesikia yale Mungu anayotwambia leo, wewe na mimi?  Atendaye dhambi ni wa Ibilisi.  Acha Roho Mtakatifu akusadikishe leo ukweli huo. 

Lakini sasa, tupate pia habari njema; Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.  Hii ndiyo sababu nyeti Yesu alikuja kwa ajili yako.  Kufuta orodha ya dhambi zako. Kuvunja kazi za Ibilisi … maishani mwako. 

Ndiyo sababu Yesu alikuja … kwa ajili yako! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.