Wakati Ile Inakuja Bila Shaka
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Ufunuo 21:22-24 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
Ebu fikiria tafadhali habari ya dunia bila jua,kasha ukosekane na mwezi. Yaani giza endelevu bila mwisho. Katika mazingira kama haya, viumbe vyote duniani vyenye uhai vingekufa haraka.
Samahani kama umeona kwamba nimeanza kipindi kwa mtazamo ulio hasi sana. Pole. Lakini usikate tamaa, mambo yatakuwa mazuri. Mazuri sana. Ebu fikiria sasa dunia ambayo haina haja tena ya jua wala mwezi; dunia ambayo mianga hiyo haihitajika tena.
Mtume Yohana alionyeshwa kidogo picha ya kule mbinguni, akitazama mara moja habari ya umilele Mungu aliotuandalia sisi ambao tunaomwamini Yesu. Hii ni picha ya sehemu ile ndogo Mungu aliyotudhihirishia kupitia yeye:
Ufunuo 21:22-24 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
Bila shaka wewe na mimi, hatuna budi kupitia siku zingine zenye giza, bila jua wala mwezi tukiishi hapa duniani. Hua zinatufikia sisi sote. Jana tuliona jinsi Yesu alikuja kuangaza nuru yake maishani mwetu. Ni jambo zuri mno!
Lakini hii ni mwanzo tu, kwa sababu ukipokea utukufu wake na kuweka tegemeo lako kwake, tayari unaingizwa katika hatima nzuri pale ambapo atakaokuwa nuru yako … milele daima. Ameshaandaa hayo tayari, ni inakungojea wewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.