... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwe na Moyo Safi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Mambo ya Nyakati 28:9 Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

Listen to the radio broadcast of

Uwe na Moyo Safi


Download audio file

Nadhani sisi sote tumewahi kutendewa jambo zuri na mtu, na isitoshe- alikutendea kwa nia njema na moyo safi kabisa.  Hii inapendeza sana.

Lakini pia, nadhani umewahi kuona mtu anakusaidia lakini kwa shingo upande.  Nia yake mbaya itadhihirika kwa maneno yake au mtazamo wake au hata kwa jinsi anavyoonekana tu.  Atafanya madogo yawezekanayo, lakini mwenye moyo mweupe atazidisha kabisa.

Wa kwanza anatukuza huduma yake wakati mtu wa pili anaishusha kana kwamba haina thamani – na kwa kufanya hivyo anafuata faida yote ya tendo lake.  Yaani ni mnafiki, si kweli?

Ndiyo maana Mfalme Daudi alitoa ushauri wenye busara kwa mwanae:

1 Mambo ya Nyakati 28:9  Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

Mungu anasikia maneno yetu yote, anaelewa mitazamo yetu, anachunguza mienendo yetu … kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira.

Unafikiri kwamba Mungu wetu ambaye yuko tayari kutusaidia wakati wa shida kwamba atafurahia nia yetu mbaya?  Je!  Atafurahia mtazamo wetu ambao unafuta kabisa maana yo yote ya tendo letukwa mwingine?

Mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote. 

Na, Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.