... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Upevu wa Kweli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 5:38,39 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.

Listen to the radio broadcast of

Upevu wa Kweli


Download audio file

Sijui ukoje, lakini mimi sipendi kuona watu wanaumizana.  Kuna wakati wanafanya makusudi, kuna wakati si kwa makusudi, Lakini kwa vyovyote vile, sisi binadamu huwa kuna wakati tunapanga jinsi ya kujilipiza kisasi.

Inakuwa hivi, Wewe na mimi, tuliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa kuwa Mungu, pamoja na kuwa Mungu wa upendo, ni Mungu wa haki pia. Na tabia hizo zote mbili, si tunafurahi kwamba awe nazo yeye kama Mwenyezi? 

Sasa kwa kuwa wewe na mimi tuliumbwa kwa sura yake, na sisi pia tumepewa uwezo mkubwa wa kupenda pamoja na kuwa na hisia ya kutaka haki itendeke. 

Lakini mtu akituumiza, kusema ukweli, asili yetu mara moja ni kutupa upendo mbali nasi na kuelekea kwenye hisia za kutafuta haki … yaani ni itikio linalofanana na upanga ukatao kuwili uwezao kutuumiza na sisi pia tukitafuta kuenenda katika njia ya kujilipiza kisasi.  Yesu alifahamu mwelekeo huo, bila shaka, ndio maana alisema hivi: 

Mathayo 5:38,39  Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. 

Hmm.  Inasemekana kwamba dalili ya mtu aliyepevuka ni pale anapoumizwa na, badala ya kumwumiza na yeye, anajaribu kumwelewa yule aliyemuumiza.  Nafikiri ndiyo lengo alilokuwa nalo Yesu pale alipotuagiza hivyo. 

Kwa sababu ukiangalia namna alivyowatendea watu kama wewe na mimi katika uasi wa dhambi zetu dhidi yake, yeye mwenyewe aligeuza shavu lake la pili kupitia kifo cha kikatili cha Yesu pale msalabani pale alipolipa deni la maovu yetu, deni lililodaiwa na haki ya Mungu. 

Geuza shavu lako la pili. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy