... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Una Matumaini Kiasi Gani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Peter 3:14,15 ... Mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.

Hivi, utaniruhusu nikuombe utulie dakika moja na kutathmini namna unavyojisikia sasa hivi; yaani hali ya hisia zako. acha nikuulize tena, Je!, Unatumaini kiasi gani … yaani unajisikia umejaa matumaini kiasi gani?

Lengo langu ni kukusaidia utambue namna unategemea mazuri au mabaya kuhusu hatima yako. Ninafahamu kwamba tuna hisia tofauti-tofauti katika vipindi mbalimbali. Lakini hisia sio za kutegemea, bado tunatambua mazingira yetu hapa duniani kupitia hisia zetu. Tunawabariki au kulaani wengine … kupitia hisia zetu.  Kwa hiyo zina umuhimu sana. 

Sasa, una moyo mkuu wenye matumaini au umekatishwa tamaa kabisa?  Ukitafakari swali langu, ebu pokea Neno la Mungu lifuatalo lenye nguvu: 

1 Peter 3:14,15  … Mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.  Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. 

Inavutia kuona nmna Mtume Petro anawaandikia Wakristo waliokuwa wanateswa vibaya akitazamia kwamba bado wanalo tumaini la kweli.  Ewe Petro, unasadiki jambo lisilohakikishwa! 

Lakini ukimtakasa Kristo moyoni mwako kuwa Bwana, ukimkazia Yesu macho, ukionea fahari msalaba wa Kristo daima; na kazi aliyokufanyia, na kujituliza katika Neno lake na kumruhusu Roho wa Mungu kuachilia uwezo wake moyoni mwako, tumaini la uhakika unalo ndani ya Yesu utafuata moja kwa moja kama vile usiku unavyofuata mchana. 

Halafu rafiki yangu, watu wanakuchunguza. Wanaona kama umekatishwa tamaa au kama una tumaini.  Ni ushuda wako kwao.  Kwa hiyo, endelea kila wakati kumtakasa Kristo kuwa Bwana moyoni mwako.  Hayo mengine lazima yatafuata tu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.