... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ujasiri Huleta Amani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 16:32,33 Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu

Listen to the radio broadcast of

Ujasiri Huleta Amani


Download audio file

Unajua kinachonipendeza zaidi nikimwangalia Yesu?  Hata kama alikuwa Mwana wa Mungu, muumba wa vitu vyote, hata kama anastahili kupata yaliyo bora kutoka kwangu na kwako pia, hawezi kutuacha tupambane peke yetu.

Wale wanafunzi kumi na wawili, waliokuwa karibu naye zaidi, walikuwa na mapungufu mengi.  Walimwangusha Yesu mara nyingi – wakibishana, wakikosa imani – na wakati ilikuwa muhimu wamtetee, kumbe walimwacha peke yake.

Lakini hata kama walifeli mara nyingi, hata kama Yesu alijua kwamba watafanya nini siku zile za mwisho akikaribia kusulubiwa, aliweza kuwaambia hivi:

Yohana 16:32,33  Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao , na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.  Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.  Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Mambo yalikuwa yanataka kuharibika mno.  Walikuwa wamemwangusha na watamwangusha tena

Ni dhairi kwamba tumemwangusha Yesu na tutamfelisha tena.  Lakini sasa hivi, mahali ulipo anatamka ujasiri wake, amani yake, mfano wake juu yetu, wewe na mimi.

Jipe moyo … yeye ameushinda ulimwengu!  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.