... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Nguvu, Upendo, Kimbilio

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 59:16 Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, nitaziimba fadhili zako kwa furaha. kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, na makimbilio siku ya shida yangu.

Listen to the radio broadcast of

Nguvu, Upendo, Kimbilio


Download audio file

umeshakukutana na mtu ambaye mambo yake yote yanaonekana kuwa sawa?  Ana ajira nzuri, ana hela za kutosha na familia inayopendeza sana.

Juzi nilikuwa ninaongea na rafiki ambaye tumejuana kwa miaka ishirini hivi.  Ni muda wa kutosha.  Yeye ni hakimu mkuu katika mahakama na jamii.  Kesi anazozisikiliza ni za ndoa kuvunjika, sababu za talaka, jinsi watoto watalelewa baada ya talaka, na mgao wa mali.

Ni mtu mwema kabisa; mwenye fadhili anayejali watu.  Ana hekima pia.  Laiti ningekuwa kama yeye.  Lakini hata mwanae amepitia msiba na maumivu ya ndoa yake kuharibika na kutenguliwa.

Kadiri ninavyozidi kuchunguza mambo, ndipo ninazidi kufikia maamuzi kwamba hakuna familia duniani ambayo haijapatwa na matatizo, mgogoro fulani, au kuharabika kwa sehemu.  Hii isingetushangaza, lakini ikitokea, bado tunashtuka, si kweli?

Je!  Ni yapi umeyapitia ambayo yamekuumiza sana?  Au ni yapi unayoyapitia sasa hivi?  Hailishi yanaonekanaje, umruhusu Mungu ayaingilie kati na kuongea na moyo wako.

Zaburi 59:16  Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, nitaziimba fadhili zako kwa furaha.  kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, na makimbilio siku ya shida yangu.

Mungu huyu, Mungu wako ni Mungu wa nguvu, wa upendo unaoonekana upya kila asuburi, ni kimbilio lako.  Rafiki yangu, yeye ni nguvu yako na usalama wako kwa sababu anakupenda. 

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.