... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ngome Zako Ziko Wapi?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 10:3-5 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tuteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.

Listen to the radio broadcast of

Ngome Zako Ziko Wapi?

Download audio file

Wakati unakutana na vizuizi njiani katika maisha haya, mwitikio wako wa haraka-haraka ni upi?  Unakumbanaje na vile vizuizi?  Ukiangalia nyuma, uliwezaje kukabiliana navyo zamani?

Vizuizi hua vinasababisha mtu asongwe na kuumia.  Katika mazingira kama hayo, tukisema ukweli, mara nyingi hatuamui vilivyo.  Pia … si kila kizuizi kilichopo nje ambavyo vinahitaji kubomelewa.  Mara nyingi kuna kizuizi kipo moyoni mwa mtu ambacho kinahitaji kushindwa kwanza.

Ebu, fikiria kwanza dhana ya ngome.  Mara nyingine tunawaza ni nguvu za giza huko sehemu fulani ambazo yatupasa kuzishinda.  Lakini labda sivyo vilivyo.

2 Wakorintho 10:3-5  Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tuteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.

Neno hilo, “ngome” linatumika mara moja tu katika Agano Jipya.  Lina maana ya mawazo ya kiburi yaliyomo mioyoni mwa waamini – kama  wewe na mimi!  Sasa ngome hizo zinajiinua juu ya elimu yetu ya kumjua Mungu.  Inatisha, si kweli?

Ndiyo maana Mungu anatuagiza tuteke nyara kila fikra ipate kumtii Kristo.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.