... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Neno la Kukumbuka

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 16:7,8 Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri, naam, mtima wangu umenifundisha usiku. Nimemweka BWANA mbele yangu daima, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.

Listen to the radio broadcast of

Neno la Kukumbuka


Download audio file

Wakati tunakumbana na matatizo, tukipambana katikati ya mazingira yaliyochafuka, hatuna budi kujisikia upweke. Labda hatuko peke yetu lakini inasikika kuwa hivyo.

Kwa kweli, kadiri mapambano yanawaka moto, kadiri tunavyozidi kuumia … ndipo inasikika kwamba Mungu ameenda mbali nasi.  Yaani, tatizo tunaokumbana nalo linaonekana kubwa mno na kumfanya Mungu kuonekana kuwa mdogo kule mbali … ikiwa bado tunaweza kumwona.  Je!  Nimeeleza hali hii kwa usahihi au?

Lakini hisia za upweke na kuwa mbali na Mungu, sio kweli kabisa.  Ukweli unaonekana katika yafuatayo:

Zaburi 16:7,8  Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri, naam, mtima wangu umenifundisha usiku.  Nimemweka BWANA mbele yangu daima, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.

Wewe na mimi, tunahitaji Roho Mtakatifu atufundishe ukweli huo, awe pamoja nasi tukigaagaa kwa fadhaa usiku.  Ndiyo maana ni muhimu sana kuwa mwanamume au mwanamke wa Neno la Mungu, ili tuweze kuwa tumejiandaa wakati shida inatujia.  Ukweli ambao tunahitaji kufundishwa na Mungu, uandikwe mioyoni mwetu – jambo lenye nguvu ambalo latupasa kukumbuka ni hili:  Nimemweka BWANA mbele yangu daima, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. 

Mfalme Daudi aliandika maneno hayo akiwa katika shida kubwa.  Lakini wakati ule, Mungu hakuonekana kuwa mbali naye kwa sababu tayari alishajua ukweli.  Rafiki yangu, Bwana daima yu pamoja nawe!

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.