Neema Iliyozidi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Yakobo 4:4-6 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Siku hizi, ni kama ni kawaida mke kuacha mume wake kwenda kwa mwingine au mume kuacha mke wake vivyo hivyo, watu wakifikiri kwamba ni maamuzi tu ya mtu. Je! Hali hii imetokea wapi?
Juzi nilisoma kibainishi kwenye mtandao kiitwacho “Jinsi ya Kufaulu katika Kutafuta Talaka.” Nilishangaa mno. Naelewa kwamba kuna nyakati talaka haiepukiki wakati kuna dhuluma izidiyo, kupigwa na kuumizwa, uasherati endelevu n.k. Hata kama haiepukiki, haipendezi.
Lakini kufanya kifungo cha ndoa kati ya mume na mke kuwa kitu chepesi hapo tukijua kwamba ni uhusiano wa muhimu kuliko yote kwa binadamu, ni jambo linalohuzunisha sana. Aliyeumizwa na uasherati wa mwenzake awaye yote atakushuhudia hivyo.
Ni vivi hivi wakati sisi, kwa upande mmoja tunakiri kwamba tunamwamini Mungu lakini kwa upande mwingine tunaonyesha mapenzi kwa kuchezea mambo ambayo anasema ni mabaya, ni kutokuwa waaminifu kwake. Ni kama uzinzi.
Yakobo 4:4-6 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Angalia. Aidha unamwamini na moyo wako wote na kuamua kumwishia uwezavyo au uache tu. Sasa, wakati mvutano kati ya tabia zako za kidunia na njia zake yeye Mungu unazidi kuwa kali, basi sikiliza! Sikiliza vizuri.
Anazidi kutupa neema, yaani anazidi kutukirimia neema. Hauko peke yako katika mapambano hayo. Stahimili.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.