... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mwawezaje Kuamini Ninyi …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 5:44 Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukutu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?

Listen to the radio broadcast of

Mwawezaje Kuamini Ninyi …


Download audio file

Sijui kama umewahi kuona utofauti kati wa matamanio yako, jinsi ungependa kuishi maisha yako na hali halisi ya maisha yako ya kila siku na mwelekeo wake ulivyo?  Kama jibu ni ndio, ujue kwamba si wewe tu.

Hali hii inaanza taratibu mtu akijisikia kwamba hana starehe lakini kadiri muda unavyoenda inaanza kuwa na maumivu makubwa.  Na kwa baadhi, kama ilivyonitokea mimi, inakuwa maumivu makali ya kulazimisha mtu kutafuta tiba.

Shida ni kwamba wakati mtu yuko kwenye mzunguko huo akisukumwa na mtazamo wa dunia hii kwamba lazima ufaulu katika yote uliyokusudia kufanya na kuanza kutimiza.  Lakini shida ni kwamba tunatumia vigezo vya mafanikio kufuatana na maoni ya watu wengine jinsi wanatupongeza au kutuonya.

Lakini ni sehemu hatari mtu akijaribu kutafuta daima utukufu kwa watu wengine, kuwa kama mtumiaji wa dawa za kulevya, daima akihitaji kupongezwa na kusikia, “Wewe ni jembe!” “Wewe ni hodari!” hii Haiwezi kujaza pengo lililomo moyoni.  Mtu ataendelea na maisha bila mwelekeo, bila malengo.  Je!  Umewahi kujisikia vitu hivi?  Siku moja Yesu alisema hivi:

Yohana 5:44  Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukutu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?

Rafiki yangu, Yesu alikuja akuweke huru na hayo yote; kuvunja vifungo vya kutaka daima utukufu wa watu na kukujaza yale yote uliyotamani kwa kumwaga utukufu wake, utukufu wa Mungu moyoni mwako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.