... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu ni Mwaminifu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:9 Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.

Listen to the radio broadcast of

Mungu ni Mwaminifu


Download audio file

Hata kama taratibu za elimu zimebadilishwa kidogo siku hizi, bado dhana ipo ya kupasi au kufeli.  Au mtu anapata maksi za kumpitisha au la.  Au anatunuliwa cheti cha kuhitimu au la.

Sasa, dhana hiyo inatumika katika sekta karibia zote za maisha.  Au unampata mwenzi na kufunga ndoa, au la.  Ndoa yako inadumu maisha yote, au la.  Unapata ajira fulani … au la.

Mwisho wa siku, ulimwengu wetu unagawika kuwili.  Kushinda au kushindwa.  Kufaulu au kufeli.  Kwa hiyo dhana hiyo tunajaribu kuitumia hata katika uhusiano wetu na Mungu.  Lakini tuwe wazi kabisa.  Ndio, msamaha wake ni karama ya neema iliolipiwa pale msalabani wakati Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu

Sasa niulize, je!  Umeishi maisha hayo kwa utimilifu wote?  Hata mimi sijafanya.  Sote tunajikwaa.  Sote bado tuna upungufu.  Je!  Ina maana kwamba tumefeli?  Hapana!  Kwa nini?  Kwa sababu …

1 Wakorintho 1:9  Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.

Katika ulimwengu huu unaogawika kuwili – yaani kushinda au kushindwa, kufaulu au kufeli, kuna jambo ambalo tunapenda kulisahau … neema ya Mungu.  Haiwezi kutuangusha, haiwezi kufeli.  Huruma zake hua zinatuonekania upya kila asubuhi.  Kamwe hawezi kushindwa kukusamehe makosa yako, mapungufu yako ya njiani wakati unamwendea na kumwomba.

Kwa sababu Yesu alilipia kila dhambi yetu – ilizopita, zilizopo sasa na hata zile tutakapozitenda baadaye.  Kwa sababu … Mungu ni mwaminifu!

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.