Makusudi Ya Moyo Wako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Wafilipi 2:3,4 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Je! Ni lini uliwahi kusema kitu au kutenda jambo ambalo, baada ya kutafakari, ulifahamu kwamba ulikosea? Sasa, ulijiuliza kwa nini ulilifanya? Mara nyingi hatujihoji. Tunaendelea mbele kasi na kurudia makosa yale yale. Kwa nini hatujifunzi lo lote?
Sisi sote tuna mazoea na tabia sugu. Mfano, kuna mtu fulani ambae humpendi, kwa hiyo wakati anakupigia simu na unaona jina lake kwenye skrini, unafuta wito wake. Ni kwa nini?
Labda utajitetea kwamba huna haja ya kuongeza shida maishani mwako siku ya leo. Huna haja kumsikiliza mtu yule akikuletea manung’uniko yake au kumsikia akikukosoa. Ni sawa, inaeleweka.
Lakini sasa acha nikuulize hivi, je! Ulikuwa na kusudi gani kwa kukataa kupokea simu yake? Ni kujilinda mwenyewe au kupuuza mtu yule msumbufu? Je! Ni kulinda amani yako au kumtia moyo kwa neno linalofaa, licha ya jinsi anavyokusumbua,
Kujihoji hivi na kuleta viulizo vihusuyo makusudi ya mioyo yetu kunatusumbua kwa kweli, lakini lazima tujipambanue. Wakati Mtume Paulo alikuwa anaeleza habari za Yesu, alisema hivi:
Wafilipi 2:3,4 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.
Halafu Mtume anaendelea kuonyesha jinsi Yesu alikubali kwenda msalabani kufa kwa ajili ya watu kama wewe na mimi, licha ya ukorofi wetu. Kwa hiyo, kwa swala la jinsi unavyowatendea wengine, daima uwe tayari kuchunguza vizuri makusudi ya moyo wako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.