Mafuriko ya Baraka
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Yohana 7:38,39 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
Je! Umewahi kujaa furaha tele – aina ya furaha ambayo inabaki ndani yako hata wakati wa shida – kiasi ambacho ulishindwa kuizuia? Labda unafikiri … Unasema nini? Furaha wakati wa shida! Labda unatania? Hapana, lakini tafadhali, chukuliana nami kwanza.
Najua kwamba ni kama kitendawili, lakini ni chungutamu ya furaha wakati wa shida, kwa kweli inapendeza moyoni. Kwa sababu wakati wa shida, kawaida tungesononeka, si kweli? Kikawaida ndivyo ilivyo, lakini si lazima iwe hivyo.
Sikukuu fulani pale Yerusalemu, Yesu alisimama na kuuambia mkutano maneno yafuatayo:
Yohana 7:38,39 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
Isitushangaze kusoma kwamba viongozi wa dini walitafuta kumwua – ilikuwa imeonekana kama alikufuru; yaani alikuwa anajilinganisha na Mungu. Lakini lengo lake lilikuwa kuonyesha kwamba uwepo wake ndio uwezayo kutujaza na mafuriko ya baraka. Si mto mmoja tu – si mto Yorodani au Frati tu, Nili au Amazoni – lakini mito mingi ya maji yaliyo hai! Roho Mtakatifu. Mungu mwenyewe kuingia wakati wenye kiu wanamjia Yesu wapate kunywa. Mito ya maji kufurika yakitutoka kwa sababu tunashindwa kuyathibiti. Mito! Furaha tele. Mafuriko ya baraka. Yaani Yesu mwenyewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.