... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maelekezo ya Kufanya Amani (1)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:12,13 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Maelekezo ya Kufanya Amani (1)


Download audio file

Kuna mambo mengi yanaweza kumkosesha mtu amani.  Lakini la kwanza kabisa ni mahusiano yetu na watu wengine.  Mfano, wakorofi.  Migogoro.  Neno kali au hata jicho la pembeni linaweza kumkosesha mtu amani.

Nadhani unajua inavyoenda.  Unaamka asubuhi ukiwa na nia njema kabisa, ukikusudia kuishi katika amani na furaha ya Bwana.  Lakini barua pepe ya kwanza unayosoma au mtu wa kwanza unayekutana naye … ghafla anabadilisha makusudi yako yote ya kutenda mema.

Amethubutu kweli!  Mimi ninastahili kuheshimiwa!  Ngoja nimwonyeshe!

Sasa mtu atafanyaje ili aweze kupitia hayo na kuishi katika amani ambayo Mungu alikusudia awe nayo?  Nikwambie kabisa kwamba yeye anataka uishi katika amani yake, uwe nayo kweli kweli.  Ni mojawapo wa mafao yake makubwa.

Wakolosai 3:12,13  Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

Unajua, mwitikio wetu dhidi ya hawa watu wanaosumbua,  ndioo…wanatukosesha amani.  Mimi ninastahili mambo bora!  Lakini ingekuaje kama tungebadilisha msimamo dhidi ya hawa wanaotukosesha amani?

 Jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu.

Hebu fikiria, ni kiasi gani cha rehema ambacho Mungu amekuonyesha?  Ni mara ngapi amekusamehe?

Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 

Huruma, utu wema, upole, msamaha … amani.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.