... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuvunja Pingu za Kale

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kumbukumbu 5:8-10 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Listen to the radio broadcast of

Kuvunja Pingu za Kale

Download audio file

Ni kitanzi kikubwa pale dhambi inarithiwa kizazi baada ya kizazi, Mtoto wa mlevi atakuwa na mwelekeo wa ulevi kuliko watoto wengine.  Mtoto aliyedhulimiwa pia, akiwa mtu mzima atakuwa na mwelekeo wa kutumia wengine vibaya.  Dhambi ya ukoo ipo kabisa.

Kweli nilikuwa na baba mzazi mzuri lakini bila mimi kujua, alikuwa anatawaliwa na michezo ya kamali.  Ni tabia aliyoificha kwangu, na ninashukuru kwa hilo, kwa sababu sikurithi vifungo hivyo. 

Lakini si hivi kila mtu, Kama tumevyoona, dhambi huwa inarithiwa kizazi baada ya kizazi. Najiuliza, umerithi matatizo gani kwenye maisha yako; unapambana na dhambi gani ya ukoo? 

Wakati bado unatafakari maswali hayo, sikiliza Neno lenye nguvu kutoka kwa Mungu: 

Kumbukumbu 5:8-10  Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.  Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 

Hapo hapo, Mungu anatupa maamuzi tuchague, ama kuendelea na dhambi ya ukoo, au kuvunja mnyororo wake; kuendelea kurithisha vizazi vinavyokuja, au kwa kutubu kwetu, kufikia mahala ambapo tunaweza kupokea mafuriko ya fadhili na baraka zake.  Ni yapi utakayochagua? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.