... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kushinda Vizuizi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 8:35-37 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.

Listen to the radio broadcast of

Kushinda Vizuizi

Download audio file

Nadhani sote tungekubaliana kinadharia kwamba mateso, tukiyapokea vilivyo, yanaweza kutengeneza na kuboresha tabia yetu.  Lakini mateso yakimfikia mtu mwenyewe, kumbe nadharia na utendaji yanaachana kabisa!

Maishani, mara nyingi, inatubidi tushinde vizuizi – madoa yaliyochafua nafsi kwenye kiini cha moyo pamoja na uvamizi unaotoka nje.

Sijui kama umeshagundua jinsi mtu anajisikia kuwa peke yake wakati anajitahidi kushinda?  Mashaka yanaingia, wengine hawaelewi unayoyapitia halafu unajisikia kwamba huna nguvu pia.

Ungesemaje nikikwambia kwamba hapo hapo uliopo unakuwa na fursa kubwa mno kutoka kwa Mungu?

Warumi 8:35-37  Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?  Je!  Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?  Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.  Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.

Mtume Paulo alikuwa anateswa vibaya sana, daima uhai wake ulikuwa hatarini wakati aliandika maneno haya.  Je!  Ungeweza kuandika hivyo katika mazingira yale?  Lakini yeye Aligundua mwenyewe kwamba katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.