... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupanga Upya Vipaumbele Vyetu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 9:36,37 Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

Listen to the radio broadcast of

Kupanga Upya Vipaumbele Vyetu


Download audio file

Kuwahudumia watu wengine ni jambo ambalo tunafahamu linafaa tulifanye.  Lakini kwa upande mwingine, mara nyingi tunaona kwamba ni usumbufu, haipendezi … hata kuwa inadhalilisha.

Mtu akitafakari kidogo, ataelewa kwamba kuhudumiana kunafanya dunia iende mbele.  Kuhudumiana kunasababisha tuishi ndani ya nyumba ambazo hatukujenga sisi wenyewe.  Tunaendesha magari ambayo tusingeliweza kuyatengeneza sisi wenyewe … hata kupiga mswaki tu, tunategemea kazi ya watu wengine.

Kikawaida, huduma hizo zinalipwa.  Mfumo huo ndio unaosukuma uchumi wa ulimwengu wetu.  Lakini huduma bora haina malipo – yaani ni bure, ila si bure kabisa, kwa kuwa inatokana na mhudumu kujitolea.

Mfano, kujitolea kwa wazazi kwa kulea watoto wao, haina malipo.  Au rafiki akija kukusaidia, hata mgeni anaweza kukuonekania na kukusaidia.  Ndiyo maana Yesu, wakati alikuwa anafundisha wanafunzi wake kuhusu ukubwa halisi aliweza kutoa mfano ufuatao …

Marko 9:36,37  Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

Kadiri tunavyowahudumia wanyonge katika jamii, walala hoi, ndipo tunamhudumia Yesu.  Kadiri tunanyosha mkono wa upendo na kujali watu wanaonekana kuwa hawafai duniani, ndipo tunamyoshea mkono Mungu wetu.

Ni yupi ambaye Mungu anakuagiza umhudumie?  Ni yupi anayekuagiza umpende na kumpokea?  Kwa sababu kadiri unayompenda na kumhudumia, na kumpokea – ndipo utakuwa unampenda na kumhudumia na kumpokea Mungu mwenyewe. 

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.