... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuoshwa Kuanzia Ndani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 51:10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.

Listen to the radio broadcast of

Kuoshwa Kuanzia Ndani


Download audio file

Mtu akitafakari kidogo, atagundua kwamba matendo yetu yanatokana moja kwa moja na mambo yanayoendela moyoni.  Shida iliyopo ni kwamba mara nyingi hatutulii na kutafakari.

Je!, Ni lini uliwahi kuhamaki?  Na Kwa nini uhamaki?  Ni kipi kilichokukosesha amani?  Yamkini ni jambo dogo lisilo na maana saana, lakini hata hivyo ulionyesha mwitikio unaolingana na mambo yaliyokuwa yanaendelea moyoni mwako wakati ule ule.

Pengine mwitikio wako ulikuwa hatua ya ziada kwenye njia uliyozoea kupita miaka nendarudi, Sasa kadiri mtu anavyozidi kusongambele katika njia hiyo, ndivyo anavyojikuta anaangukia katika mwenendo wa uharibifu unaomfunga.

Ilikuwa hivi maishani mwa Daudi, mfalme wa Israeli zamani wakati alipozini na mke wa mtu mwingine na kusababisha auawe.  Baada ya kugundua kwamba uovu huu mkubwa umetokea moyoni mwake, akijua ya kwamba hakuwa na uwezo wowote wa kujithibiti, basi alipaza sauti na kuomba hivi: 

Zaburi 51:10  Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.

Kubadilisha kiini cha moyo wako ni kazi ngumu mno kabisa, na mara nyingi haiwezekani hata kidogo.  Kwa hiyo Daudi alikuwa na busara ya kumwomba Mungu abadilishe moyo wake; kujishughulisha na kazi ya kumwosha moyoni; kutumia Roho wake Mtakatifu kuleta mabadiliko yanayofaa kutokana na moyo uliobadilishwa na Mungu mwenyewe.

kweli, Daudi alitumia hekima kuomba hivyo, badala ya kujaribu kubadilisha matendo yake mwenyewe wakati moyo wake ulikuwa bado hauko sawa.

Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.