... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kubadilishwa na Utukufu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 3:18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.

Listen to the radio broadcast of

Kubadilishwa na Utukufu


Download audio file

Ninajiuliza, ukiangalia nyuma maishani mwako, ni yapi ambayo yamekutengeneza na kukubadilisha uwe mtu kama ulivyo leo?  Ni watu gani, mahusiano gani, mazingira gani hata majaribu pamoja na baraka gani ambavyo vimekufinyanga?

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la kujiona kwamba hawafai kwa sababu ya jinsi walivyotendewa wakati walikuwa wadogo.  Walionusurika kutoka kwenye mazingira ya dhuluma bado wanayo majeraha yanayowaathiri.  Bila shaka kuna mahusiano mengi yasiyofaa pamoja na matukio mabaya yaliyowabadilisha hawa watu.

Kwa upande mwingine, mtu aliyekulia katika nyumba salama akiwa na wazazi wanaompenda – hajailishi kama ni matajiri au maskini – bila shaka atakuwa na mtazamo tofauti kabisa ya ulimwengu na nafasi aliyo nayo ndani yake.

Kwangu mimi, ilikuwa mchanganyiko.  Wazazi wazuri sana, nyumba salama, elimu nzuri, lakini nilikuwa na kiburi kupita kiasi, kiburi ambacho kiliweza kuharibu kabisa sehemu kubwa ya ujana wangu.  Lakini hatimaye, siku moja yenye giza nene, yaani siku mbaya yenye upweke na maumivu makubwa, Yesu alinionekania na mambo yakaanza kubadilika.

2 Wakorintho 3:18  Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.

Wakati utukufu wa Mungu unaangazia moyoni mwako kupitia Yesu, Mwana wake Mungu, utukufu wake utakubadilisha; utakuponya; utakujaza nuru na raha na furaha na amani kwa jinsi isiyoweza kuelezeka.  Halafu kadiri utakavyomsogelea Yesu, ndipo atazidi kukubadilisha, kutoka utukufu hadi kiwango kingine cha utukufu.

Yesu anabadilisha kila kitu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy