... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Inatosha Kabisa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 12:8,9 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

Listen to the radio broadcast of

Inatosha Kabisa


Download audio file

Je!  Umewahi kubana kidole chako kwenye mlango?  Mambo yalikuwa shwari halafu ghafla maumivu yanapanda mkono na kuingia kichwani kwa ukali kabisa.  Yaani inaumiza mno!

Sehemu zingine za mwili wako ziko sawa.  Hata mambo yako yote mengine maishani yanaweza kuwa mazuri lakini mawazo yako yote yametekwa na maumivu yale makali wakati kucha yako inaanza kugeuka kuwa rangi ya blu.

Hata wakati wa maumivu makali yanaanza kupoa baada ya dakika kumi hivi, bado maumivu endelevu yatakusumbua mchana kutwa usiweze kufurahia siku ile.

Ni vivyo hivyo kwa jambo hilo moja maishani mwako, jambo ambalo unatamani lisiwepo.  Kila mtu ana shida sugu ile moja, ikiwa hii au ile.  Zamani, Mtume Paulo alikuwa na mwiba mwilini mwake – yaani mwiba ubavuni kama inavyosemakana.  Aliuelezea kama ifuatavyo:

2 Wakorintho 12:8,9  Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.  Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha;  maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.  Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

Hata ukikabiliana ni jambo gani, neema ya Mungu yakutosha.  Daima ilikuwa hivyo.  Na itaendelea kuwa hivyo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy