... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Imani Yako Ishindayo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 11:29-34 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa. Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba. Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani. Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walinshida milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.

Listen to the radio broadcast of

Imani Yako Ishindayo


Download audio file

Acha nikutupie hoja, nione unafikiriaje.  Mkristo awaye yote asipotambua kwamba tunaishi katika eneo la vita ya kiroho ni kama haelewi cho chote Kabisa!  Sasa, wewe unaonaje?

Kuridhika kupita kiasi ni adui kabisa ya maisha mapya tuliyopokea kutokana na kifo na ufufuo wa Yesu.  Labda wengine hawatapendezwa kuyasikia, lakini ndiyo sababu watu wa Mungu wengi wanakosa kufurahia maisha tele yenye baraka Mungu alizokusudia kwa ajili yao.

Lakini turudi nyuma kidogo.  Ingekuaje kama wana wa Israeli wasingevuka Mto Yorodani na kuingia katika Nchi ya Ahadi?

Waebrania 11:29-34  Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa.  Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba.  Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani.  Nami niseme nini tena?  Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga.  Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.

Israeli hawakuingia Nchi ya Ahadi hivi hivi tu.  Iliwalazimu kuipigania … mapigano baada ya mapigano.  Angalia pia habari ya watu wa Mungu waliotajwa katika Maandiko yale.  Kuenenda kwa imani inamaanisha kupiga vita, mapigano baada ya mapigano.

Ndivyo ilivyokuwa tangu zamani.  Usiridhike kupita kiasi na hali yako ilivyo.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.