Huruma za Baba Mzazi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Zaburi 103:13,14 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.
Juzi tulikuwa tumemwalika rafiki yetu wa karibu kuja kula nasi jioni. Kijana wake na mkazana wake walikuwa wanatazamia kuzaa mtoto. Lakini katikati ya chakula, alipigiwa simu na mke wake, akimwambia taarifa za huzuni mno.
Sikuweza kusikia yaliyoongelewa, lakini kwa kuangalia sura yake, mara moja nilijua kilichotokea. Mkazana wake alikuwa meporomosha mimba; mtoto alipotea.
Yaani muda ule ule, sura yake ilionyesha wazi kilichokuwa moyoni mwake. Ilikuwa huruma za baba mzazi, kwa ajili ya watoto wake, kwa ajili ya maumivu na hasara waliyoipata.
Na hata kama tukio lenyewe lilikuwa la huzuni mno, huruma za yule baba ndizo zilizotakiwa zidhihirike kwa kipindi kigumu kile. Kwa sababu huruma ya mzazi si ya kugushi.
Zaburi 103:13,14 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.
Ni rahisi sana katika mapambano ya maisha kusahau ukweli wa huruma za Mungu kwako, Kwa moyo wake mkubwa kama Baba mzazi, anakuonea shauku, anaumia sana kwa ajili yako. Anasikia maumivu yote unayopata kana kwamba ameumia yeye … hata kama maumivu yale yanatokana na makosa yako wewe mwenyewe. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi ni mavumbi.
Kwahiyo, unapoumia, unapojikuta katikati ya msiba mzito, kumbuka ya kwamba … upendo wa Mungu kwako. Ni kweli. Ni kweli halisi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.