... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hofu ya Kutokukubaliwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 12:42,43 Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi. Kwa maana walipenda utukutu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Hofu ya Kutokukubaliwa


Download audio file

Kuogelea kinyume na mkondo wa mto, yaani kusimama kidete kuhusu jambo ambalo rafiki zako, jamaa na jamii kwa ujumla hawakubaliani nalo ni jambo gumu kabisa.  Ndiyo, watu wengi hawako tayari kuonyesha msimamo.

Hata kama siku hizi kuna mfumo wa mtu kuonyesha kwamba ana msimamo kwenye mada ya kisasa, hususani katika siasa, kuwa na msimamo kutenda yaliyo haki kinyume na uovu, kwa kweli itamgharimu mtu sana.

Willima Tyndale alichomwa moto mwaka wa 1536 kwa kosa la kutafsiri Biblia kutoka Kilatini kuiweka katika Kiingereza tu.  Mwaka wa 1972 mwinjilisti wa Kichina aitwaye Watchman Nee aliuawa kwa kuwaambia watu habari za Yesu.  Kwa kweli, kumekuwa wafia dini wengi sana katika karne hii moja iliyopita kuliko waliofia dini wote katika makarne 19 kabla ya hapo.

Daima kumekuwa gharama kubwa kwa kusimama kidete kinyume cha mtazamo wa umma.  Hata wakati Yesu alikuwepo hapa duniani …

Yohana 12:42,43  Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.  Kwa maana walipenda utukutu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.

Ndiyo hali halisi, si kweli?  Kujali zaidi mawazo ya watu wengine kuliko kufuata dhamiri ya moyoni kumwamini Yesu.  Ni kwa sababu njia rahisi ni kuendana na mtazamo wa wengine.  Kuamini sirini au hata kupelekwa mbali na Mungu kabisa.

Ni kweli, kuna watu wengi duniani hawana budi kuamini sirini.  Lakini sisi wengine, tukimwacha Yesu kwa sababu ya mawazo ya watu wengine itakuwa kwa sababu tunapenda kupokea utukufu kutoka binadamu wenzetu na kufarijika kwao kwa muda mfupi kuliko kutafuta utukufu utokao kwa Mungu utakaoendelea milele daima. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.