... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Halafu Siku Ile …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Malaki 4:2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.

Listen to the radio broadcast of

Halafu Siku Ile …


Download audio file

Nafikiri wengi wetu tunaona kama kutoa mahesabu ni jambo jema. Kila mtu anapaswa kuwajibika kwa mwenendo wake. Lazima thawabu ziwepo kwa ajili ya mema na adhabu kwa ajili ya maovu … si kweli?

Jana tuliona namna wanaotenda maovu duniani wanapinga kabisa dhana ya kwamba kuna hukumu ya Mungu, wakikana uwepo wa mbingu na jehanamu pia … hata kama hawaamini kwamba vipo.  Lakini tusidanganyike, Mungu atawalazimisha watoe hesabu yote ya waliyoyatenda. 

Malaki 4:1  Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.  

Lakini kwa upande wa pili itakuaje?  Watakuwaje wale wanaoishi kwa kumheshimu Mungu?  Itakuaje kwao siku ile ya hukumu inayokuja? 

Malaki 4:2  Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.

Hapa pia mwandishi anatumia picha inayogonga sana. Sijui kama umewahi kuwepo pale wanapofuga ng’ombe halafu asubuhi jua linapochomoza ndama huwa zinaanza kuruka-ruka zikitoka zizini … yaani ni tukio linaloashiria furaha kuliko mengine yote mtu angefikiria. 

Ndivyo uzima ulivyo kwa ajili ya watu wanaolicha jina la Mungu, wenye kuishi kwa ajili ya kumtukuza kwa jinsi wanavyoweza, wale wanaokaza mwendo wa kumfuata Yesu kama mmoja wa wanafunzi wake. 

Kwahiyo, kama wewe ni mmoja wao, Mungu amekusudia kukubariki kwa furaha isiyotamkwa, kuanzia sasa … hadi milele daima.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.