... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Chunguza Neno la Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 4:12,13 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.

Listen to the radio broadcast of

Chunguza Neno la Mungu

Download audio file

Je!  Uliwahi kujiuliza kwa nini unapambana na mambo yanayokusumbua?  Bwana na Bibi Wakristo Wakamilifu huko hawasumbuliwi.  Lakini mimi?  Si unajua …

Ni kawaida mtu kujiliganisha na wengine hivi, asijue hata kidogo mapambano waliyo nayo wao.  Lakini kuna wakati tunajiletea matatizo sisi wenyewe kwa kwenda mbali na Mungu na mbali na Neno lake. tukijidanganya kwamba sisi tunajua, kwamba mapungufu yetu hayawezi kutuathiri wala hayana matokeo mabaya.

Lakini kule kujidanganya kumbe ni kifaa mkononi mwa Shetani kupora mali ambayo Mungu alitaka kutukirimia kwayo.  Na bila kukwepa, kuna njia moja tu ya kurudi:

Waebrania 4:12,13  Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.  Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.

Mchungaji wa Kikristo aitwaye Jack Wellman alijumlisha mistari hiyo miwili hivi:  “Ukilichunguza Neno la Mungu, utakuta kwamba ni Neno la Mungu ndilo linakuchunguza wewe!”  Na kwa kufanya hivyo, Mungu anabainisha jinsi tunavyojidanganya na dhambi ili Ibilisi aliyepitia kwa kupora maisha yetu.  Lengo la Mungu ni kutuweka huru na kutuonyesha pendo lake na kutuvuta kwake kuliko tulivyowahi kufikiria inawezekana.

Usiache Neno la Mungu.  Lina nguvu ya kubadilisha mtu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.