Azimio la Amani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Warumi 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Kuna watu wengi sana ambao wanatumia nguvu nyingi za kihisia kwa kujaribu kukimbia yaliyotokea zamani, bila hata kujua wanachokifanya. Mimi nilikuwa hivi miaka mingi iliyopita. Je! Na wewe uliwahi kuwa hivi?
Kukimbia mambo yaliyopita, yaani matendo mabaya uliyoyafanya, au yale uliyotendewa, kunachosha na kumchanganya mtu. Mtu anataka kuishi maisha bora, lakini kwa njia moja au nyingine majuto ya zamani yanamkosesha amani.
Naweza kueleza hali hiyo kwa usahihi kwa sababu niliipitia mwenyewe. Hatimaye niligundua kwa kuchelewa kwamba kitu kimoja ambacho nilikuwa ninakikimbia kilikuwa Mungu mwenyewe. Mle ndani ya fikra zangu hata kwenye kiini cha moyo wangu nilijua kwamba kuna Mungu anayenipenda, lakini nilikuwa na aibu kabisa kwa sababu ya yale yote niliyoyafanya na tabia nilizozijenga maishani. Vipi wewe, ulishapitia hali kama hiyo?
Siku moja, wakati niliingia kanisani shingo upande, mhubiri alisimama na kubainisha vizuri Habari Njema ya Yesu. Halafu Habari hiyo Njema ni hii, kwamba …
Warumi 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Hii ni zaidi ya Habari Njema, ni Habari Njema Mno – kwako wewe, kwangu mimi. Tumehesabiwa haki mbele za Mungu kupitia imani yetu ndani ya Yesu, na kupitia yeye, hatimaye, tunayo amani kwa Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.